Baada ya kupata chanjo yako | After your vaccination

Unachoweza kuhisi Kinachoweza kusaidia Wakati hii inaweza kuanza
Maumivu mahali ambapo sindano imedungwa, maumivu ya kichwa na kuhisi uchovu.

Haya ni madhara yanayoripotiwa sana.
Weka kwa muda mfupi kitambaa baridi, chenye unyevunyevu, au barafu mahali ambapo umedungwa sindano.

Usisugue au kukanda mahali ambapo umedungwa sindano.
Ndani ya saa 6 hadi 24 
Maumivu ya misuli, kujihisi mgonjwa, baridi, homa, maumivu ya viungo na kichefuchefu pia kinaweza kutokea. Pumzika na unywe maji mengi.

Unaweza kumeza paracetamol au ibuprofen, fuata maagizo ya mtengenezaji.

Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wako wa afya ikiwa dalili zako zinazidi kuwa mbaya.
Ndani ya saa 6 hadi 48 


Kama ilivyo kwa dawa zote, chanjo inaweza kusababisha madhara kwa baadhi ya watu. Hivi ndivyo mwili unakabiliana kwa kawaida na inaonyesha kuwa chanjo inafanya kazi.

Kwa kawaida madhara huwa sio kali, hayadumu kwa muda mrefu na hayatakuzuia kupata kipimo cha pili au kufanya shughuli zako za kila siku.

Madhara yanaweza kutokea zaidi baada ya dozi yako ya pili ya chanjo.

Athari mbaya za mzio zinaweza kutokea lakini ni nadra sana. Watoa chajo wa Nyuzilandi wamefundishwa kuzidhibiti. Madhara mengine yanaweza kuathiri kwa muda mfupi uwezo wako wa kuendesha au kutumia mashine. Jambo hilo nadra linapofanyika, tafadhali jadiliana na mwajiri wako.

Ukipata dalili ambazo zinaweza kuwa zinahusiana na COVID-19, kukohoa kwa muda mrefu, halijoto ya juu/homa au upotezaji au mabadiliko katika hisi yako ya kawaida ya ladha au kunusa, kaa nyumbani na upimwe COVID-19.

Ikiwa una athari isiyotarajiwa ya chanjo yako ya COVID-19, anayekupa chanjo au mtaalamu wa afya anapaswa kuripoti kwa Kituo cha Kufuatilia Athari Mbaya (Centre for Adverse Reactions Monitoring - CARM).

Unaweza pia kuripoti athari zozote zisizotarajiwa kwa kutumia fomu yao ya kuripoti mtandaoni kwenye tovuti ya CARM: otago.ac.nz/carm (external link).

Ikiwa huna uhakika kuhusu dalili zako au ikiwa zinaendelea kuwa mbaya, piga simu kwa
0800 358 5453.

Ikiwa una wasiwasi wa haraka kuhusu usalama wako, piga simu kwa 111, na hakikisha umewaambia umepata chanjo ya COVID-19 ili waweze kukutathmini vizuri.

Chanjo husaidia kulinda watu wa kila kizazi dhidi ya magonjwa mengine ya kuambukiza pia, kama surua na flu.

Angalia ikiwa wewe na whānau wako mnapata chanjo kwa wakati unaofaa kwa kuzungumza na mtoa huduma wenu wa afya. Tembelea health.govt.nz/immunisation (external link) ili kupata maelezo zaidi.

Unahitaji kusubiri angalau wiki mbili baada ya kipimo chako cha pili cha chanjo ya COVID-19 kabla ya kupata chanjo nyingine yoyote.